Hata Mbuyu ulianza kama mchicha
Sisi watu wafuatao
tumeanzisha Mfuko huu ambao utakuwa ukijishughulisha na majanga yanayowakabili
wanachama wake pamoja na jamii kwa ujumla. Majanga hayo ni kama vile, vifo,
ajali, mafuriko yataokanayo na mvua, upepo utakaosababisha majanga ya kukosa
makazi au kuharibu makazi ya mmoja wa wanachama wa mfuko huu.
Pia utakuwa
ukijishughulisha na kusaidia katika hali ya mambo ya kijamii, kama vile kuoa na
kuolewa, kuozesha mtoto, kusomesha mtoto, na kujisaidia katika bishara ndogo
ndogo ili kujikwamua kutokana na umasikiniwa kipato nk.
Wanachama waanzilishi wa mfuko huu ni
hawa wafuatao:
A.
|
JINA
|
KIINGILIO
|
1.
|
ESTHER DAFFA
|
50,000.00
|
2.
|
EMMA SIZYA
|
50,000.00
|
3.
|
SAUDA RAJABU
|
50,000.00
|
4.
|
ESTER MSECHU
|
50,000.00
|
5.
|
ASHA WAHINDI
|
50,000.00
|
6.
|
STEVEN ANTHONY
|
50,000.00
|
7.
|
JOYCE SAMWEL
|
50,000.00
|
8.
|
FATUMA KILENGA
|
50,000.00
|
9.
|
SAADA MYINGA
|
50,000.00
|
10.
|
DEVOTA ELISAE
|
50,000.00
|
11.
|
LUSAJO MWAKASEGE
|
50,000.00
|
12.
|
SUBIRA WADDA
|
50,000.00
|
13.
|
SHABANI KALUSE
|
50,000.00
|
14.
|
VICTORIA GUNZE
|
50,000.00
|
15.
|
ALICE KASHILILILA
|
50,000.00
|
16.
|
GETRUDA FLORIAN
|
50,000.00
|
17.
|
FATUMA MSIGALA
|
50,000.00
|
18.
|
JOSEPH MWITA
|
50,000.00
|
19.
|
JACKSON MUMBII
|
50,000.00
|
20.
|
FLOLENCE MAREALE
|
50,000.00
|
JUMLA TSHS.
|
1,000,000.00
|
Dhamira yetu:
Kuhakikisha wanachama wote wanahudumiwa
kwa uwazi na kwa uhakika na pia kuhakikisha kwamba tunaepuka kuwa na ukiritimba
utakaowafanya wanachama wa mfuko huu kupoteza imani na kikundi chao.
Uadilifu:
Kuhakikisha kwamba
wanachama wote bila kujali nafasi zao za uongozi wanaiheshimu katiba ya kikundi
hiki na wanakuwa na maadili ya kutovunja
sheria za kikundi na za nchi kwa ujumla
Taaluma:
Wanachama wa kikundi
hiki watatekeleza wajibu tuliojiwekea kwa ubora, uwezo, uwajibikaji na upendo
wa hali ya juu wakati wote na pia kuwawezesha wanachama kushiriki kikamilifu
katika shughuli za uongozi wa kikundi kwa kuwajengea uwezo wa kushiriki katika
shughuli mbalimbali za kikundi zikiwemo zile za kiuchumi
Uwazi:
Shughuli za kikundi
hiki zitakuwa zinaendeshwa kwa uwazi na kutoa taarifa kikamilifu ili
kuwawezesha wanachama wa kikundi hiki kunufaika na mfuko wao.
Uaminifu:
Shughuli za kikundi hiki zitakuwa
zikiendeshwa kwa uaminifu wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment