Wednesday, August 8, 2012

NGOME IMARA NI NINI.........?

Hata Mbuyu ulianza kama mchicha

Sisi watu wafuatao tumeanzisha Mfuko huu ambao utakuwa ukijishughulisha na majanga yanayowakabili wanachama wake pamoja na jamii kwa ujumla. Majanga hayo ni kama vile, vifo, ajali, mafuriko yataokanayo na mvua, upepo utakaosababisha majanga ya kukosa makazi au kuharibu makazi ya mmoja wa wanachama wa mfuko huu.

 Pia utakuwa ukijishughulisha na kusaidia katika hali ya mambo ya kijamii, kama vile kuoa na kuolewa, kuozesha mtoto, kusomesha mtoto, na kujisaidia katika bishara ndogo ndogo ili kujikwamua kutokana na umasikiniwa kipato nk.

Wanachama waanzilishi wa mfuko huu ni hawa wafuatao:

A.
JINA
KIINGILIO
1.
ESTHER DAFFA
50,000.00
2.
EMMA SIZYA
50,000.00
3.
SAUDA RAJABU
50,000.00
4.
ESTER MSECHU
50,000.00
5.
ASHA WAHINDI
50,000.00
6.
STEVEN ANTHONY
50,000.00
7.
JOYCE SAMWEL
50,000.00
8.
FATUMA KILENGA
50,000.00
9.
SAADA MYINGA
50,000.00
10.
DEVOTA ELISAE
50,000.00
11.
LUSAJO MWAKASEGE
50,000.00
12.
SUBIRA WADDA
50,000.00
13.
SHABANI KALUSE
50,000.00
14.
VICTORIA GUNZE
50,000.00
15.
ALICE KASHILILILA
50,000.00
16.
GETRUDA FLORIAN
50,000.00
17.
FATUMA MSIGALA
50,000.00
18.
JOSEPH MWITA
50,000.00
19.
JACKSON MUMBII
50,000.00
20.
FLOLENCE MAREALE
50,000.00
JUMLA TSHS.
1,000,000.00

 Dhamira yetu:
Kuhakikisha wanachama wote wanahudumiwa kwa uwazi na kwa uhakika na pia kuhakikisha kwamba tunaepuka kuwa na ukiritimba utakaowafanya wanachama wa mfuko huu kupoteza imani na kikundi chao.

Uadilifu:
Kuhakikisha kwamba wanachama wote bila kujali nafasi zao za uongozi wanaiheshimu katiba ya kikundi hiki na  wanakuwa na maadili ya kutovunja sheria za kikundi na za nchi kwa ujumla

Taaluma:
Wanachama wa kikundi hiki watatekeleza wajibu tuliojiwekea kwa ubora, uwezo, uwajibikaji na upendo wa hali ya juu wakati wote na pia kuwawezesha wanachama kushiriki kikamilifu katika shughuli za uongozi wa kikundi kwa kuwajengea uwezo wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kikundi zikiwemo zile za kiuchumi

Uwazi:
Shughuli za kikundi hiki zitakuwa zinaendeshwa kwa uwazi na kutoa taarifa kikamilifu ili kuwawezesha wanachama wa kikundi hiki kunufaika na mfuko wao.
Uaminifu:

Shughuli za kikundi hiki zitakuwa zikiendeshwa kwa uaminifu wa hali ya juu.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...