Wednesday, September 26, 2012

MUHTASARI WA KIKAO CHA KWANZA CHA KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIANA KILICHOFANYIKA SIKU YA IJUMAA TAREHE 15/6/2012

MUHTASARI WA KIKAO CHA  KWANZA CHA KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIANA KILICHOFANYIKA SIKU YA IJUMAA  TAREHE 15/6/2012 KWENYE HOTEL YA SERENA DAR ES SALAAM

1.0       MAHUDHURIO
          A:      WALIOHUDHURIA
S/N
JINA
WADHIFA
1.
ESTHER DAFFA
MJUMBE
2.
EMMA SIZYA
MJUMBE
3.
SAUDA RAJABU
MJUMBE
4.
ESTER MSECHU
MJUMBE
5.
ASHA WAHINDI
MJUMBE
6.
NEEMA ABDALLAH
MJUMBE
7
JOYCE SAMWEL
MJUMBE
8
FATUMA KILENGA
MJUMBE
9
DEVOTA ELISAE
MJUMBE
10
LUSAJO MWAKASEGE
MJUMBE
11
SUBIRA WADDA
MJUMBE
12
SHABANI KALUSE
MJUMBE
13
FLOLENCE MAREALE
MJUMBE
14
ALICE KASHILILILA
MJUMBE
15
GETRUDA FLORIAN
MJUMBE
16
FATUMA MSIGALA
MJUMBE


B:  WASIOHUDHURIA  - 

S/N
JINA
WADHIFA
1
JOSEPH MWITA
MJUMBE
2
JACKSON MUMBII
MJUMBE
3
SAADA MUYINGA
MJUMBE
4
VICTORIA GUNZE
MJUMBE



2.0       UFUNGUZI WA KIKAO

Mjumbe aliyeitisha kikao Sauda Rajabu aliwashukuru wajumbe wote kwa mahudhurio yao kwenye  kikao hicho na alitangaza kukifungua rasmi kikao cha kwanza.
3.0       AGENDA
KULIKUWA NA AGENDA TATU ZA KUJADILIWA KATIKA KIKAO HICHO
1.   Kujadili juu ya kuanzishwa kwa mfuko wa kusaidiana
2.   Kujadili jina la kikundi
3.   Kuteua kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi
4.   Mengineyo

3.1  AGENDA NAMBA 1
Kujadili juu ya kuanzishwa kwa kikundi cha kusaidianana na kutungwa kwa katiba:
Wajumbe tulikubaliana juu ya kuanzisha mfuko wa kusaidiana wakati wa majanga yanapotokea miongoni mwa jamii zetu. Kutokana na mazingira yetu ya kazi, kwani muda mwingi tunautumia hapa kazini na kushiundwa kushirikiana na jamii iliyotuzunguka huko mitaani tunapoishi tumejikuta tunakuwa katika wakati mgumu wa kuyakabili majanga hayo, ambayo aidha hutokea kwa uasilia wake au kwa bahati mbaya.

Pia tumeangalia hali ngumu ya maisha inayo zikabili jamii nyingi hapa Dar es Salaam na Nchini kwa ujumla na kwamba   Jamii nyingi kukosa mitaji ya kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa kujiongezea kipato na kukidhi baadhi ya mahitaji muhimu ya kibanadamu.

Pia tulijadili juu ya kutungwa kwa katiba ya kikundi ambayo itazingatia mambo yafuatayo:

-          mwanachama kuacha kazi/kujitoa
-          Mwanachama akiuguliwa atasaidiwaje (atapewa fedha kiasi gani)
-          Mwanachama akifunga ndoa atasaidiwaje na kikundi
-          Mwanachama akifiwa na watu wake wa karibu au msiba kuwepo nyumba anayoishi.
-          Kufungua Account ya kikundi
-          Jinsi ya kuunganisha Chama na uongozi wa hoteli ili michango yetu ikatwe moja kwa moja kutoka kwenye mshahara na kwenda bank moja kwa moja badala ya kushikana mashati.
-          Mahudhurio ya kikao, wanachama wajitahidi kuhudhuria, hakuta kuwa na lawama kwa wasio hudhururia kwa lolote litakaloamuliwa na kikao au wanachama waliokuwepo.
-          Kuwezeshana kimtaji ianze haraka iwezekanavyo kwa lengo la kukuza kikundi hasa upande wa riba.
-           Kuanzia siku ya leo mwanachama yoyote atakaye patwa na tatizo kubwa wanachana wanawajibu wa kuwajibika kama kikundi kumsaidia ikiwa ndio dhana kubwa ya kuanzishwa kwa kikundi hichi.
-          Ikitokea mwanachama amepatwa na tatizo kubwa kabla ya mfuko kutuna wanachama watatakiwa kuchanga kutoka kwenye mifuko yao kwaajili ya kumsaidia mwanachama mwenzao.
-          Fain itatolewa kwa watakao kuwa wanachelewa kwenye kikao au kutohudhuria mara kwa mara kwenye vikao pasipo sababu maalum.
-          Maendelea yanayolengwa kwa ajili ya baadae yawekwe kabisa katika katiba ili kuondoa usumbufu hapo baadae, kama ujasiliamali n.k.
-          Kwa kuanza ifunguliwa Account  ya kawaida , watu wawili waijue password kwakuwa pesa haziwezi kuwa zinakaa mfukoni kwa mtu ni” risk”.
-          Kwa sasa jambo litakalo hitaji pesa kama utengenezaji wa katiba n.k uchakavu upitishwe.
-          Baada ya kukamilika kwa katiba kila mwanachama atahitajika kuwa na katiba na aisome na kuielewa ili tuwe kwenye mstari mmoja.
-          Kuwepo na kamati ndogo ndogo ndani ya kikundi K.M kamati ya misiba,harusi n.k.
-          Kamati hizo ndizo zitaleta taarifa ya matumizi ya pesa na yatakayojiri sehemu husika.
-          Kwa baadae atakayetaka kujinga na kikundi imependekezwa ada iwe ni sh laki mbili, ili kupunguza msongamano wa kuwa na wanachama wengi.
-          Kiingilio kwa wanachama ishirini wa mwanzo ni sh 5000/= na mchango  wa kila mwezi ni 5000/=, michango inatakiwa kuanza kutolewa June, na kiingilio kinatakiwa kuwa kimekamilika mwishoni mwa mwezi wa saba.
3.2  AGENDA NAMBA 2
Kujadili jina la kikundi:
Wajumbe walikubaliana kila mmoja apendekeze jina la kikundi ambapo wajumbe waliomba wapewe muda wa kutafakari, hata hivyo muumbe mmoja Shaban Alipendekeza jina la kikundi liwe ni NGOME IMARA.
Wajumbe wote waliridhia jina hili lipitishwe kwa muda lakini kama kutakuwa na pendekezo la jina lingine, basi liwasilishwe kwenye mkutano wa pili wa kikundi kwa ajili ya kupigiwa kura.

3.3  AGENDA NAMBA 3
Kuteua kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi:

Wajumbe walipendekeza majina ya wajumbe sita kuingia kwenye kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi na kuiwasilisha kwenye mkutano mkuu wa pili wa kikundi ambapo kamati hiyo ilipwea mwezi mmoja kukamilisha rasimu hiyo ya katiba.

Wajumbe hao waliochaguliwa na nafasi zao ni hawa wafuatao:

Jina la mjumbe
Wadhifa
Shaban Kaluse
Mwenyekiti
Sauda Rajabu
Makamu mwenyekiti
Emma Sizya
Katibu
Devota Elisea
Katibu msaidizi
Esther Daffa
Mweka hazina
Ester Msechu
Mweka hazina msaidizi


Mwenyekiti wa muda aliyeteuliwa akizungumza na wajumbe wa kikao hicho aliwashukuru kwa kumuamini na kumteua kuongoza jahazi hilo la kuanza rasimu ya kikundi. Pia kwa niaba ya wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo, mwenyekiti alieleza hatua za awali za kuchukua katika utekelezaji wa kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Mwenyekiti alitaka wajumbe waanze kutoa michango yao ili pamoja na mambo mengine ituwezeshe kufanikisha uandaaji wa rasimu hiyo ya katiba na pia kulipia gharama za usajili. Wajumbe walikubaliana na wazo hilo na mwenyekiti aliwaomba watoe mapendekezo yao.

Makamu mwenyekiti Sauda Rajabu alitoa maoni kwamba kila mwanachama atoe kiingilio cha shilingi 50,000 halafu michango kwa mwezi iwe ni shilingi 5,000 kila mwezi.

Wajumbe waliafiki, lakini waliomba kiasi hicho cha shilingi 50,000 kisitolewe kwa mkupuo kwa sababu ya hali ngumu walizo nazo wajumbe waanzilishi. Ilikubaliwa kishi hicho kilipwe kwa awamu mbili ikiwa ni sambamba  na mchango wa kila mwezi wa silingi 5,000. Hivyo basi iloiamuliwa mwisho mwezi wa Juni kila mwanachama atoe kiasi cha shilingi 25, 000 pamoja na shilingi 5,000 ya mcnago wa mwezi jumla itakuwa ni shilingi 30,000, halafu na mwisho  wa mqwezi wa Julai wajumbe wote watoe kiashi hicho hicho.
Wajumbe wpte waliafiki wazo hilo na kulipitisha.

3.4  AGENDA NAMBA 4.
Mengineyo:
Hapakuwa na hoja zaidi na kila mjumbe aliridhishwa makubalianao hayo.
4.0     KUFUNGA KIKAO
Mwenyekiti aliwashukuru  wajumbe wote kwa michango yao ya mawazo katika kikao hicho.
Aliwakumbusha  wajumbe kuweka vyema kumbukumbu za kikao hicho ili kuepusha kusahau maazimio waliyoyafanya wakati wa kikao hicho.

Kikao kijacho kitakuwa tarehe 15/06/2012.

Alitamka kukifunga  rasmi kikao cha 1 cha kikundi cha NGOME IMARA.



16 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...