1.0 MAHUDHURIO
A: WALIOHUDHURIA
S/N
|
JINA
|
WADHIFA
|
1.
|
ESTHER DAFFA
|
MWEKA HAZINA WA MUDA
|
2.
|
SAUDA RAJABU
|
MAKAMU MWENYEKITI WA MUDA
|
3.
|
JOSEPH MWITA
|
MJUMBE
|
4.
|
JACKSON MUMBII
|
MJUMBE
|
5.
|
SAADA MUYINGA
|
MJUMBE
|
6.
|
JOYCE SAMWEL
|
MJUMBE
|
7.
|
DEVOTA ELISEA
|
KATIBU MSAIDIZI WA MUDA
|
8.
|
SUBIRA WADDA
|
MJUMBE
|
9.
|
SHABANI KALUSE
|
MWENYEKITI WA MUDA
|
10.
|
FLOLENCE MAREALE
|
MJUMBE
|
11.
|
ALICE KASHILILILA
|
MJUMBE
|
12.
|
GETRUDA FLORIAN
|
MJUMBE
|
13.
|
FATUMA MSIGALA
|
MJUMBE
|
B: WASIOHUDHURIA -
JINA
|
WADHIFA
|
|
1.
|
ESTER MSECHU
|
MWEKA HAZINA MSAIDIZI WA MUDA
|
2.
|
ASHA WAHINDI
|
MJUMBE
|
3.
|
NEEMA ABDALLAH
|
MJUMBE
|
4.
|
FATUMA KILENGA
|
MJUMBE
|
5.
|
LUSAJO MWAKASEGE
|
MJUMBE
|
6.
|
VICTORIA GUNZE
|
MJUMBE
|
7.
|
EMMA SIZYA
|
KATIBU WA MUDA
|
B: MGENI MWALIKWA
JINA
|
WADHIFA
|
|
1.
|
STEVEN ANTHONY
|
MWENYEKITI CHODAWU DAR SERENA HOTEL
|
2.0 UFUNGUZI
WA KIKAO
Katibu msaidizi Devota Elisea alimkaribisha mwenyekiti ili
afungue kikao hicho.
Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe waliohudhuria kikao hicho na
alichuku nafasi hiyo kumtambulisha mgeni mwalikwa ndugu Steven Anthony
mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi hapa Hotelini Serena (CHODAWU. Mwenyekiti
alieleza sababu za kumwalika mwenyekiti huyo wa (CHODAWU) kwamba kwanza ni
kutaka afahamu kuhusu kikundi chetu na pili ni ni
kutaka atoe maoni yake juu ya katiba yetu na mwisho awe ndiye msimamizi wa
uchaguzi mkuu wa kikundi.
1.6 AGENDA
KULIKUWA
NA AGENDA KUMI ZA KUJADILIWA KATIKA KIKAO HICHO
NA
|
AGENDA
|
1
|
Kufungua Mkutano
|
2
|
Taarifa ya mwenyekiti wa muda
|
3
|
Uchaguzi wa viongozi wa kikundi pamoja na viongozi wa
kamati za kikundi
|
4
|
Mwenyekiti mpya kukabidhiwa majukumu na kuendesha mkutano
|
5
|
Kusoma na kupitisha ya viwango vya misaada ya kwa
wanachama kwa Mwaka 2012/2013
|
6
|
Kuwasilisha taarifa ya makisio ya bajeti ya kila kamati kwa
mwaka 2012/2013
|
7
|
Uchaguzi wa kamati mbalimbali za kikundi na kukabidhi
majukumu kwa kila kamati
|
8
|
Kuteua wajumbe watakaokuwa wanatia sahihi katika benki
|
9
|
Kiwango cha michango
cha mwezi
|
10
|
Mengineyo
|
3.1 AGENDA YA KWANZA
Kufungua Mkutano:
Baada ya kusoma agenda
za kikao Mwenyekiti alifungua kikao rasmi saa 9:00.
3.2 AGENDA
YA PILI
Taarifa ya mwenyekiti
wa muda:
Mwenyekiti
alitoa taaarifa yake kuhusiana na kazi aliyopewa na wajumbe wenzake, awali ya
yote aligawa rasimu ya katiba kwa wajumbe wote kisha akaeleza matumizi
yaliyotumika mpaka kufikia hatua hiyo ambapo alitoa mchanganuo wa matumizi hayo
yaliyofikia kiasi cha shilingi 77,000.
Aliwaomba
wajumbe wapokee taarifa hiyo, na kama kuna mwenye hoja ajitokeze. Wajumbe wote
waliafiki taarifa hiyo. Hatua iliyofuata ikiongozwa na katibu msaidizi ilikuwa
ni kupitia rasimu ya katiba ambapo wajumbe wote waliafiki kwamba katiba iko
sahihi na waliridhika nayo.
Kabla
kumkaribisha mwenyekiti wa chodawu wa Serena Hotel, mwenyekiti alitangaza rasmi
kuvunja kamati yake ili kupisha uchaguzi mkuu, ambapo alimkaribisha mwenyekiti
wa chodawu na alimuomba kwamba pamoja na kuwa msimamizi wa uchaguzi, lakini pia
atoe nasaha zake.
Viongozi
wote wa kamati waliondoka katika meza kuu na kuungana na wajumbe wengine wa
kikundi kwa ajili ya kufanya uchaguzi mkuu.
3.3 AGENDA
YA TATU
Uchaguzi
wa viongozi wa kikundi pamoja na viongozi wa kamati za kikundi:
Kabla
ya kuanza kwa uchaguzi mkuu, msimamizi wa uchaguzi, ndugu Steven Anthony
alionyesha kufurahishwa kwake na wazo la wajumbe wa kikao hicho kuanzisha mfuko
wa kuwawezesha kukabiliana na hali za majanga na matatizo ya kiuchumi.
Aliwaomba
wajumbe ikiwezekana wafungue milango kwa wafanyakazi wengine wenye nia ya
kujiunga na kikundi hiki kwani ni wafanyakazi wachache waliobuni wazo hilo,
lakini Hoteli ina jumla ya wafanyakazi wapato 350 hadi 400 ambapo kuna
uwezekano mkubwa wa wafanyakazi wengi wakawa na nia ya kutaka kujiunga na mfuko
huo.
Pia
aliomba kama ikiwezekana kiwango cha michango kwa mqwezi kiongezwe kutoka
shilingi 5,000 hadi shilingi 20,000 ili kuufanya mfuko uwe imara na kuwawezesha
wafanyakazi kupata misaada mbalimbali pale watakapokabiliwa na matatizo.
Baada
ya kusema hayo mwenyekiti huyo wa CHODAWU aliitisha uchaguzi rasmi.
Nafasi zilizokuwa
zikigombewa ni hizi zifuatazo:
i. MWENYEKITI WA MFUKO
ii. MAKAMU MWENYEKITI
iii. KATIBU MKUU
iv. NAIBU KATIBU MKUU
v. MWEKA HAZINA
vi. MWEKA HAZINA MSAIDIZI
i. MWENYEKITI WA MFUKO
ii. MAKAMU MWENYEKITI
iii. KATIBU MKUU
iv. NAIBU KATIBU MKUU
v. MWEKA HAZINA
vi. MWEKA HAZINA MSAIDIZI
Utaratibu uliokubaliwa na wanachama wote ni kila mwanachama aandike majina sita wakiyagawa katika makundi ya wawili wawili yaani nafasi ya mwenyekiti na msaidizi wake waandike majina mawili na nafasi ya katibu na msaidizi wake pia wapendekeze majina mawili hivyo hivyo na nafasi ya mweka hazina na msaidizi wake.
Msimamizi
wa uchaguzi aligawa karatasi za kura na kila mjumbe alipiga kura na kurejesha
karatasi hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi ambapo matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Nafasi ya mwenyekiti
na msaidizi wake
No.
|
Jina
|
Nafasi aliyopendekezwa
|
Idadi ya kura
|
1.
|
Shaban Kaluse
|
Mwenyekiti
|
13
|
2.
|
Sauda Rajabu
|
Makamu Mwenyekiti
|
9
|
3.
|
Devota Elisea
|
Makamu mwenyekiti
|
2
|
4.
|
Joseph Mwita
|
Makamu Mwenyekiti
|
1
|
5.
|
Jackson Mumbii
|
Makamu Mwenyekiti
|
1
|
Nafasi ya katibu na
msaidizi wake
No.
|
Jina
|
Nafasi aliyopendekezwa
|
Idadi ya kura
|
1.
|
Jackson Mumbii
|
Katibu
|
2
|
2.
|
Sauda Rajabu
|
Katibu Msaidizi
|
3
|
3.
|
Devota Elisea
|
Katibu Msaidizi
|
9
|
4.
|
Emma Sizya
|
Katibu
|
11
|
*Kura moja iliharibika
Nafasi ya Mweka Hazina
na msaidizi wake
No.
|
Jina
|
Nafasi aliyopendekezwa
|
Idadi ya kura
|
1.
|
Joyce Samuel
|
Mweka hazina msaidizi
|
1
|
2.
|
Joseph Mwita
|
Mweka hazina
|
1
|
3.
|
Esther Daffa
|
Mweka hazina
|
12
|
4.
|
Ester Msechu
|
Mweka hazina msaidizi
|
12
|
Viongozi
waliochaguliwa kwa kura na nafasi zao ni hawa wafuatao:
No.
|
Jina
|
Wadhifa
|
Idadi ya kura
|
1.
|
Shaban Kaluse
|
Mwenyekiti
|
13
|
2.
|
Sauda Rajabu
|
Makamu mwenyekiti
|
9
|
3.
|
Emma Sizya
|
Katibu
|
11
|
4.
|
Devota Elisea
|
Katibu msaidizi
|
9
|
5.
|
Esther Daffa
|
Mweka hazina
|
12
|
6.
|
Ester Msechu
|
Mweka hazina msaidizi
|
12
|
Msimamizi wa uchaguzi aliuita kwenye meza kuu uongozi mpya
wa kikundi na kuupongeza kisha akamkaribisha katibu aendelee na kikao.
3.4 AGENDA
YA NNE
Uongozi mpya kukabidhiwa majukumu na kuendesha mkutano:
Katibu anamkaribisha mwenyekiti ili aendelee na kikao.
Mwenyekiti mpya akizungumza na wajumbe wa kikao hicho
aliwashukuru kwa kumuamini na kumchagua kuongoza kikundi hicho. Pia kwa niaba
ya viongozi wenzake waliochaguliwa, mwenyekiti aliwapongeza na kuwataka
kuhakikisha kwamba hatuwaangushi wana NGOME
IMARA kwani wanayo matarajio
makubwa sana kutoka katika uongozi waliotulkabidhi
Pia aliwapongeza wajumbe ambao kura hasikutosha lakini
aliwataka wasidhani kwamba hawaaminiwi na wajumbe wa mkutano huo mkuu, bali ni
katika kutekeleza demokrasia.
3.5 AGENDA
YA TANO
Kusoma na kupitisha ya viwango vya misaada ya kwa
wanachama kwa
Mwaka 2012/2013:
Kama
madhumuni ya kuanzishwa kwa mfuko huu yalivyoainishwa katika katiba mfuko huu
utakuwa ni kwa ajili ya kusaidiana wakati wa maafa na majanga yatakayo na hali
iliyo nje ya hali za kawaida na kuwakumba wanakikundi wa mfuko huu, maafa na
majanga hayo ni kama vile; Vifo, ajali, mafuriko yatokanayo na
mvua, Upepo utakao sababisha majanga ya kukosa makazi na kuharibu makazi ya
mmojawapo katika mfuko, moto nk.
Kusaidiana
katika hali ya mambo ya kijamii kama vile Kuoa na kuolewa, kuozesha mtoto,
kukopesha wanachama wake kwa ajili ya kusomesha mtoto, na kujisaidia katika
biashara ndogondogo ili kujikwamua kutokana na umasikini wa kipato nk.
2. MISIBA:
Mtu aliyefariki
|
Kiwango cha mchango
|
Baba mzazi
|
200,000
|
Mama mzazi
|
200,000
|
Baba mkwe
|
200,000
|
Mama mkwe
|
200,000
|
Mke/Mume
|
300,000
|
Mwanachama
|
500,000 pamoja na 50% ya michango yake
|
Mtoto wa mwanachama
|
300,000
|
3. SHEREHE:
Aina ya Sherehe
|
Kiwango cha mchango
|
Kuoa
|
300,000
|
Kuolewa
|
300,000
|
Kuozesha/Kuoza
|
200,000
|
Kuzaliwa mtoto
|
200,000
|
4. MISAADA MBALIMBALI YA MAJANGA:
AINA YA JANGA
|
KIWANGO CHA MSAADA
|
Kuunguliwa na nyumba
|
500,000
|
Kukumbwa na mafuriko
|
200,000
|
Mwanachama kupata
ajali na kulazwa hospitalini inayomlazimu kukaa nje ya kazi kwa muda mrefu
au Mwanachama kuugua
kwa muda mrefu au kuuguliwa na mume mke au mtoto wa kumzaa mwenywe kwa muda
mrefu
|
200,000
|
BAJETI
YA MWAKA YA KIKUNDI KULINGANA NA MICHANGO YA WANACHAMA NA ITAANZA KUTUMIKA
KUANZIA JULY 2012 MPAKA
JULY 2013
Bajeti hii itakuwa
ikipitiwa kila baada ya miezi mitatu na kufanyiwa marekebisho kulingana na
mapato ya kikundi
AINA YA MATUMIZI
|
KIASI KILICHOTENGWA
|
KIASI KILICHOTUMIKA
|
KIASI KILICHOBAKI
|
Misiba
|
1000,000
|
||
Sherehe
|
1000,000
|
||
Misaada ya majanga
|
1000,000
|
||
Mikopo ya dharura
|
2000,000
|
||
Jumla
|
5000,000
|
Bajeti ni nakisi tu ya
gharama ambazo zinaweza kutumika kulingana na matumizi yaliyokusudiwa na
kuafikiwa na wanakikundi. Kila kamati italazimika kupitia bajeti yake kila
baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa katiba na kuandika ripoti ambayo
itawasilishwa kwenye kamati ya utendaji. Kama kamati yoyote itakayokuwa
imepungukiwa na fedha kutokana na matumizi inaweza kuomba fedha nyingine kutoka
kwa mweka hazina ikiambatanisha maombi hayo na mchanganuo wa matumizi ya bajeti
iliyopita. Iwapo akaunti ya kikundi itakuwa haina fedha zan kutosha, Mweka
hazina anaweza kukopa kutoka katika bajeti za kamati nyingine kama tu kamati
hizo zitakuwa na fedha za kutosha kufanya hivyo.
4.6 AGENDA SITA
Uchaguzi
wa kamati mbalimbali za kikundi na kukabidhi majukumu kwa kila kamati
Kwa mujibu wa katiba
kutakuwa na kamati tano zitakazokuwa zikifanya kazi kwwa mujibu wa katiba.
Wajumbe kwa pamoja
walichagua wajumbe wa kamati hizo kama ifuatavyo:
Kamati
ya Utendaji- Hii ndio itakuwa kama hub ya kikundi itakuwa
ndiyo chombo kikuu cha utendaji wa shughuli zote za mfuko za kila
siku kama zitakavyo elekezwa na mkutano mkuu, pamoja na majukumu yake ya msingi
kamati Utendaji itasimamia na kupokea taarifa mbali mbali za kama nyingine na
kuziwasilisha katika kikao cha mkutano mkuu wa kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.
Kamati
hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
|
Jina
|
Wadhifa
|
1.
|
Shaban Kaluse
|
Mwenyekiti
|
2.
|
Emma Sizya
|
Katibu
|
3.
|
Joseph Mwita
|
Mjumbe
|
4.
|
Saada Myinga
|
Mjumbe
|
5.
|
Asha Wahindi
|
Mjumbe
|
Kamati ya Maafa- itawajibika
kwa kamati ya utendaji ya mfuko, pamoja na mambo mengine kamati itafanya vikao
vyake kila mwezi mara moja na kupitia taarifa zote zinazohusiana na maafa kwa
ujumla wake na kujadili ukubwa wa tatizo au maafa pale ambapo mfuko haujaweka
bayana kiwango stahiki kwa maafa ya namna hiyo kwa mwanachama na kisha
kuwasilisha mapendekezo yake kwa kamati ya utendaji ya mfuko kwa maidhinisho ya
malipo stahiki.
Kamati hii itakuwa na
wajumbe wafuatao:
No.
|
Jina
|
Wadhifa
|
1.
|
Jackson Mumbii
|
Mwenyekiti
|
2.
|
Devota Elisea
|
Katibu
|
3.
|
Subira Wada
|
Mjumbe
|
4.
|
Getrude Florian
|
Mjumbe
|
5.
|
Neema Abdallah
|
Mjumbe
|
Kamati
ya tathmini ya misaada na maafa ya mfuko:
Kutakuwa na kamati ya tathimini ya mfuko
ambayo itakuwa ikikutana mara moja kwa mwezi na pia kukutana kwa vikao vya
dharaura itakapo lazimu haja ya kufanya hivyo wakati wowote wa mwanzo wa
mwezi na kwa matukio
yoyote ya kati ya mwezi yatakuwa yakisubiri mwisho wa mwezi kwa kingizwa katika
agenda za kikao cha mwezi. Pamoja na mambo mengine kamati itawajibika kwa
Kamati ya Utendaji ya Mfuko na Itapokea taarifa za maafa na majanga toka kwa
kamati ya maafa na kuyafanyia tathimini ya kweli kwa uzito wa janga husika.
Pia itakapokea taarifa za misaada toka
kwa kamati ya misaada ya jamii kama itakavyowasilishwa kwake na kuifanyia
uchambuzi na tathimini sahihi juu ya misaada inayoombewa fedha/msaada husika.
Kamati
hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
|
Jina
|
Wadhifa
|
1.
|
Sauda Rajabu
|
Mwenyekiti
|
2.
|
Joseph Mwita
|
Katibu
|
3.
|
Victoria Gunze
|
Mjumbe
|
4.
|
Lusajo Kasege
|
Mjumbe
|
5.
|
Fatuma Kilenga
|
Mjumbe
|
6.
|
Esther Daffa
|
Mjumbe
|
Kamati ya huduma za kijamii: Kutakuwa na kamati ya huduma za jamii itakayo kutana kila mwezi mara moja na itawajibika kwa kamati ya Utendaji ya Mfuko: Ipatopkea maombi mbali mbali ya misada toka kwa wanachama na kuyajadili kisha kuyatolea mapendekezo yake kwa Kamati ya tathimini ya Misaada na Maaafa ya mfuko kwa utekelezaji wa hatua ya kufanyiwa tathimini juu ya maombi husika. Kamati itafanya uhakiki wa ukubwa wa tatizo la mwanachama linaloombewa misaada kabla ya kuliwasilisha na kulitolea mapendekezo yake kwa kamati ya tathimini ya misaada na maafa ya mfuko.
Kamati hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
|
Jina
|
Wadhifa
|
1.
|
Devota Elisea
|
Mwenyekiti
|
2.
|
Esther Msechu
|
Katibu
|
3.
|
Fatuma Msigalla
|
Mjumbe
|
4.
|
Alice Kashililika
|
Mjumbe
|
5.
|
Victoria Gunze
|
Mjumbe
|
6.
|
Florence Mariale
|
Mjumbe
|
7.
|
Joyce Samueli
|
Mjumbe
|
Kamati
ya Nidhamu ya mfuko: Kutakuwa na kamati ya NIDHAMU ya
mfuko ambayo pamoja na majukumu yake mengine ya msingi, kamati itakuwa
ikikutana mara moja kwa mwezi na kujadili hali ya nidhamu ya wanachama na
kuchukuwa hatua za awali juu ya mwanachama atakeyeonekana amekiuka miiko ya
uongozi na/au kufanya tendo lolote la kumdhalilisha mwanachama mwenzake,
viongozi wake au kwenda kinyume na MAADILI, DIRA,
NA DHIMA ya Mfuko.
Kamati
hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
|
Jina
|
Wadhifa
|
1.
|
Shaban Kaluse
|
Mwenyekiti
|
2.
|
Lusajo Kasege
|
Katibu
|
3.
|
Fatuma Kilenga
|
Mjumbe
|
4.
|
Saada Myinga
|
Mjumbe
|
5.
|
Devota Elisea
|
Mjumbe
|
6.
|
Emma Sizya
|
Mjumbe
|
4.0 AGENDA YA SABA.
Kuteua
wajumbe watakaokuwa wanatia sahihi katika benki;
Waliteuliwa
wajumbe watatu wa kutia saini katika Benki, mweka hazina anaingia katika orodha
hii kwa mujibu wa katiba.
Watia
saini ni hawa wafuatao:
No.
|
Jina
|
Wadhifa
|
1.
|
Shaban Kaluse
|
Mwenyekiti
|
2.
|
Esther Daffa
|
Mweka Hazina
|
3.
|
Devotha Elisea
|
Katibu Msaidizi
|
8.0 AGENDA YA NANE.
Mengineyo:
Hapakuwa
na hoja zaidi na kila mjumbe aliridhishwa makubalianao hayo.
9.0 AGENDA YA TISA.
Wajumbe
walikubaliana kubadilisha kiwango cha michango kwa mwezi, kutoka shilingi 5,000
hadi shilingi 10.000. Hiyo ni kutokana na kuitikia wito wa Mwenyekiti wa
Chodawu Serena Dar es Salaam Ndugu Steven Anthony aliyeshauri tuongeze kiwango
cha michango cha mwezi ikiwezekana kiwe shilingi 20,000. Wajumbe walikubaliana
na ushauri huo.
10.0 AGENDA YA KUMI.
KUFUNGA
KIKAO
Mwenyekiti
aliwashukuru wajumbe wote kwa michango yao ya mawazo katika kikao
hicho.
Aliwakumbusha wajumbe
kuweka vyema kumbukumbu za kikao hicho ili kuepusha kusahau maazimio
waliyoyafanya wakati wa kikao hicho.
Alitamka
kukifunga rasmi kikao cha 2 cha kikundi cha NGOME
IMARA saa 12:00 jioni