Wednesday, September 26, 2012

MUHTASARI WA MKUTANO MKUU WA PILI WA KIKUNDI CHA NGOME IMARA WA KUPITISHA RASIMU YA KATIBA YA KIKUNDI NA KUFANYA UCHAGUZI MKUU KILICHOFANYIKA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 19/7/2012 KWENYE HOTEL YA SERENA DAR ES SALAAM

1.0       MAHUDHURIO
A:      WALIOHUDHURIA
S/N
JINA
WADHIFA
1.
ESTHER DAFFA
MWEKA HAZINA WA MUDA
2.
SAUDA RAJABU
MAKAMU MWENYEKITI WA MUDA
3.
JOSEPH MWITA
MJUMBE
4.
JACKSON MUMBII
MJUMBE
5.
SAADA MUYINGA
MJUMBE
6.
JOYCE SAMWEL
MJUMBE
7.
DEVOTA ELISEA
KATIBU MSAIDIZI WA MUDA
8.
SUBIRA WADDA
MJUMBE
9.
SHABANI KALUSE
MWENYEKITI WA MUDA
10.
FLOLENCE MAREALE
MJUMBE
11.
ALICE KASHILILILA
MJUMBE
12.
GETRUDA FLORIAN
MJUMBE
13.
FATUMA MSIGALA
MJUMBE


 B:  WASIOHUDHURIA  

JINA
WADHIFA
1.
ESTER MSECHU
MWEKA HAZINA MSAIDIZI WA MUDA
2.
ASHA WAHINDI
MJUMBE
3.
NEEMA ABDALLAH
MJUMBE
4.
FATUMA KILENGA
MJUMBE
5.
LUSAJO MWAKASEGE
MJUMBE
6.
VICTORIA GUNZE
MJUMBE
7.
EMMA SIZYA
KATIBU WA MUDA

B:  MGENI MWALIKWA
JINA
WADHIFA
1.
STEVEN ANTHONY
MWENYEKITI CHODAWU DAR SERENA HOTEL


2.0       UFUNGUZI WA KIKAO

Katibu msaidizi Devota Elisea alimkaribisha mwenyekiti ili afungue kikao hicho.
Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe waliohudhuria kikao hicho na alichuku nafasi hiyo kumtambulisha mgeni mwalikwa ndugu Steven Anthony mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi hapa Hotelini Serena (CHODAWU. Mwenyekiti alieleza sababu za kumwalika mwenyekiti huyo wa (CHODAWU) kwamba kwanza ni kutaka afahamu kuhusu kikundi chetu na pili ni  ni kutaka atoe maoni yake juu ya katiba yetu na mwisho awe ndiye msimamizi wa uchaguzi mkuu wa kikundi.

          1.6        AGENDA
KULIKUWA NA AGENDA KUMI ZA KUJADILIWA KATIKA KIKAO HICHO

NA
AGENDA
1
Kufungua Mkutano
2
Taarifa ya mwenyekiti wa muda
3
Uchaguzi wa viongozi wa kikundi pamoja na viongozi wa kamati za kikundi
4
Mwenyekiti mpya kukabidhiwa majukumu na kuendesha mkutano
5
Kusoma na kupitisha ya viwango vya misaada ya kwa wanachama  kwa Mwaka 2012/2013
6
Kuwasilisha taarifa ya makisio ya bajeti ya kila kamati kwa mwaka 2012/2013
7
Uchaguzi wa kamati mbalimbali za kikundi na kukabidhi majukumu kwa kila kamati
8
Kuteua wajumbe watakaokuwa wanatia sahihi katika benki
9
Kiwango cha michango cha mwezi
10
Mengineyo

3.1 AGENDA YA KWANZA
Kufungua Mkutano:
Baada ya kusoma agenda za kikao Mwenyekiti alifungua kikao rasmi saa 9:00.
3.2 AGENDA YA PILI
Taarifa ya mwenyekiti wa muda:
Mwenyekiti alitoa taaarifa yake kuhusiana na kazi aliyopewa na wajumbe wenzake, awali ya yote aligawa rasimu ya katiba kwa wajumbe wote kisha akaeleza matumizi yaliyotumika mpaka kufikia hatua hiyo ambapo alitoa mchanganuo wa matumizi hayo yaliyofikia kiasi cha shilingi 77,000.
Aliwaomba wajumbe wapokee taarifa hiyo, na kama kuna mwenye hoja ajitokeze. Wajumbe wote waliafiki taarifa hiyo. Hatua iliyofuata ikiongozwa na katibu msaidizi ilikuwa ni kupitia rasimu ya katiba ambapo wajumbe wote waliafiki kwamba katiba iko sahihi na waliridhika nayo.
Kabla kumkaribisha mwenyekiti wa chodawu wa Serena Hotel, mwenyekiti alitangaza rasmi kuvunja kamati yake ili kupisha uchaguzi mkuu, ambapo alimkaribisha mwenyekiti wa chodawu na alimuomba kwamba pamoja na kuwa msimamizi wa uchaguzi, lakini pia atoe nasaha zake.
Viongozi wote wa kamati waliondoka katika meza kuu na kuungana na wajumbe wengine wa kikundi kwa ajili ya kufanya uchaguzi mkuu.
3.3 AGENDA YA TATU
Uchaguzi wa viongozi wa kikundi pamoja na viongozi wa kamati za kikundi:
Kabla ya kuanza kwa uchaguzi mkuu, msimamizi wa uchaguzi, ndugu Steven Anthony alionyesha kufurahishwa kwake na wazo la wajumbe wa kikao hicho kuanzisha mfuko wa kuwawezesha kukabiliana na hali za majanga na matatizo ya kiuchumi.
Aliwaomba wajumbe ikiwezekana wafungue milango kwa wafanyakazi wengine wenye nia ya kujiunga na kikundi hiki kwani ni wafanyakazi wachache waliobuni wazo hilo, lakini Hoteli ina jumla ya wafanyakazi wapato 350 hadi 400 ambapo kuna uwezekano mkubwa wa wafanyakazi wengi wakawa na nia ya kutaka kujiunga na mfuko huo.
Pia aliomba kama ikiwezekana kiwango cha michango kwa mqwezi kiongezwe kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 20,000 ili kuufanya mfuko uwe imara na kuwawezesha wafanyakazi kupata misaada mbalimbali pale watakapokabiliwa na matatizo.
Baada ya kusema hayo mwenyekiti huyo wa CHODAWU aliitisha uchaguzi rasmi.
Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni hizi zifuatazo:
   i.      MWENYEKITI WA MFUKO
 ii.     MAKAMU MWENYEKITI
iii.    KATIBU MKUU
iv.     NAIBU KATIBU MKUU
v.      MWEKA HAZINA
vi.     MWEKA HAZINA MSAIDIZI

Utaratibu uliokubaliwa na wanachama wote ni kila mwanachama aandike majina sita wakiyagawa katika makundi ya wawili wawili yaani nafasi ya mwenyekiti na msaidizi wake waandike majina mawili na nafasi ya katibu na msaidizi wake pia wapendekeze majina mawili hivyo hivyo na nafasi ya mweka hazina na msaidizi wake.
Msimamizi wa uchaguzi aligawa karatasi za kura na kila mjumbe alipiga kura na kurejesha karatasi hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi ambapo matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Nafasi ya mwenyekiti na msaidizi wake
No.
Jina
Nafasi aliyopendekezwa
Idadi ya kura
1.
Shaban Kaluse
Mwenyekiti
13
2.
Sauda Rajabu
Makamu Mwenyekiti
9
3.
Devota Elisea
Makamu mwenyekiti
2
4.
Joseph Mwita
Makamu Mwenyekiti
1
5.
Jackson Mumbii
Makamu Mwenyekiti
1

Nafasi ya katibu na msaidizi wake
No.
Jina
Nafasi aliyopendekezwa
Idadi ya kura
1.
Jackson Mumbii
Katibu
2
2.
Sauda Rajabu
Katibu Msaidizi
3
3.
Devota Elisea
Katibu Msaidizi
9
4.
Emma Sizya
Katibu
11


*Kura moja iliharibika

Nafasi ya Mweka Hazina na msaidizi wake
No.
Jina
Nafasi aliyopendekezwa
Idadi ya kura
1.
Joyce Samuel
Mweka hazina msaidizi
1
2.
Joseph Mwita
Mweka hazina
1
3.
Esther Daffa
Mweka hazina
12
4.
Ester Msechu
Mweka hazina msaidizi
12


Viongozi waliochaguliwa kwa kura na nafasi zao ni hawa wafuatao:
No.
Jina
Wadhifa
Idadi ya kura
1.
Shaban Kaluse
Mwenyekiti
13
2.
Sauda Rajabu
Makamu mwenyekiti
9
3.
Emma Sizya
Katibu
11
4.
Devota Elisea
Katibu msaidizi
9
5.
Esther Daffa
Mweka hazina
12
6.
Ester Msechu
Mweka hazina msaidizi
12


Msimamizi wa uchaguzi aliuita kwenye meza kuu uongozi  mpya wa kikundi na kuupongeza kisha akamkaribisha katibu aendelee na kikao.

3.4  AGENDA YA NNE
Uongozi mpya kukabidhiwa majukumu na kuendesha mkutano:

Katibu anamkaribisha mwenyekiti ili aendelee na kikao.
Mwenyekiti mpya akizungumza na wajumbe wa kikao hicho aliwashukuru kwa kumuamini na kumchagua kuongoza kikundi hicho. Pia kwa niaba ya viongozi wenzake waliochaguliwa, mwenyekiti aliwapongeza na kuwataka kuhakikisha kwamba hatuwaangushi wana NGOME IMARA kwani wanayo matarajio makubwa sana kutoka katika uongozi waliotulkabidhi

Pia aliwapongeza wajumbe ambao kura hasikutosha lakini aliwataka wasidhani kwamba hawaaminiwi na wajumbe wa mkutano huo mkuu, bali ni katika kutekeleza demokrasia.

3.5  AGENDA YA TANO
Kusoma na kupitisha ya viwango vya misaada ya kwa wanachama  kwa Mwaka 2012/2013:
Kama madhumuni ya kuanzishwa kwa mfuko huu yalivyoainishwa katika katiba mfuko huu utakuwa ni kwa ajili ya kusaidiana wakati wa maafa na majanga yatakayo na hali iliyo nje ya hali za kawaida na kuwakumba wanakikundi wa mfuko huu, maafa na majanga hayo ni kama vile;  Vifo, ajali, mafuriko yatokanayo na mvua, Upepo utakao sababisha majanga ya kukosa makazi na kuharibu makazi ya mmojawapo katika mfuko, moto nk.

Kusaidiana katika hali ya mambo ya kijamii kama vile Kuoa na kuolewa, kuozesha mtoto, kukopesha wanachama wake kwa ajili ya kusomesha mtoto, na kujisaidia katika biashara ndogondogo ili kujikwamua kutokana na umasikini wa kipato nk.

2.   MISIBA:
Mtu aliyefariki
Kiwango cha mchango
Baba mzazi
200,000
Mama mzazi
200,000
Baba mkwe
200,000
Mama mkwe
200,000
Mke/Mume
300,000
Mwanachama
500,000 pamoja na 50% ya michango yake
Mtoto wa mwanachama
300,000

3.   SHEREHE:
Aina ya Sherehe
Kiwango cha mchango
Kuoa
300,000
Kuolewa
300,000
Kuozesha/Kuoza
200,000
Kuzaliwa mtoto
200,000


4.   MISAADA MBALIMBALI YA MAJANGA:
AINA YA JANGA
KIWANGO CHA MSAADA
Kuunguliwa na nyumba
500,000
Kukumbwa na mafuriko
200,000
Mwanachama kupata ajali na kulazwa hospitalini inayomlazimu kukaa nje ya kazi kwa muda mrefu au  Mwanachama kuugua kwa muda mrefu au kuuguliwa na mume mke au mtoto wa kumzaa mwenywe kwa muda mrefu
200,000


BAJETI YA MWAKA YA KIKUNDI KULINGANA NA MICHANGO YA WANACHAMA NA ITAANZA KUTUMIKA KUANZIA JULY 2012  MPAKA JULY 2013
Bajeti hii itakuwa ikipitiwa kila baada ya miezi mitatu na kufanyiwa marekebisho kulingana na mapato ya kikundi

AINA YA MATUMIZI
KIASI KILICHOTENGWA
KIASI KILICHOTUMIKA
KIASI KILICHOBAKI
Misiba
1000,000
Sherehe
1000,000
Misaada ya majanga
1000,000
Mikopo ya dharura
2000,000
Jumla
5000,000

Bajeti ni nakisi tu ya gharama ambazo zinaweza kutumika kulingana na matumizi yaliyokusudiwa na kuafikiwa na wanakikundi. Kila kamati italazimika kupitia bajeti yake kila baada ya miezi mitatu kwa mujibu wa katiba na kuandika ripoti ambayo itawasilishwa kwenye kamati ya utendaji. Kama kamati yoyote itakayokuwa imepungukiwa na fedha kutokana na matumizi inaweza kuomba fedha nyingine kutoka kwa mweka hazina ikiambatanisha maombi hayo na mchanganuo wa matumizi ya bajeti iliyopita. Iwapo akaunti ya kikundi itakuwa haina fedha zan kutosha, Mweka hazina anaweza kukopa kutoka katika bajeti za kamati nyingine kama tu kamati hizo zitakuwa na fedha za kutosha kufanya hivyo.

4.6        AGENDA SITA
Uchaguzi wa kamati mbalimbali za kikundi na kukabidhi majukumu kwa kila kamati

Kwa mujibu wa katiba kutakuwa na kamati tano zitakazokuwa zikifanya kazi kwwa mujibu wa katiba.

Wajumbe kwa pamoja walichagua wajumbe wa kamati hizo kama ifuatavyo:

Kamati ya Utendaji- Hii ndio itakuwa kama hub ya kikundi itakuwa ndiyo chombo kikuu cha utendaji wa shughuli zote za mfuko za  kila siku kama zitakavyo elekezwa na mkutano mkuu, pamoja na majukumu yake ya msingi kamati Utendaji itasimamia na kupokea taarifa mbali mbali za kama nyingine na kuziwasilisha katika kikao cha mkutano mkuu wa kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Kamati hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
Jina
Wadhifa
1.
Shaban Kaluse
Mwenyekiti
2.
Emma Sizya
Katibu
3.
Joseph Mwita
Mjumbe
4.
Saada Myinga
Mjumbe
5.
Asha Wahindi
Mjumbe


Kamati ya Maafa- itawajibika kwa kamati ya utendaji ya mfuko, pamoja na mambo mengine kamati itafanya vikao vyake kila mwezi mara moja na kupitia taarifa zote zinazohusiana na maafa kwa ujumla wake na kujadili ukubwa wa tatizo au maafa pale ambapo mfuko haujaweka bayana kiwango stahiki kwa maafa ya namna hiyo kwa mwanachama na kisha kuwasilisha mapendekezo yake kwa kamati ya utendaji ya mfuko kwa maidhinisho ya malipo stahiki.

Kamati hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
Jina
Wadhifa
1.
Jackson Mumbii
Mwenyekiti
2.
Devota Elisea
Katibu
3.
Subira Wada
Mjumbe
4.
Getrude Florian
Mjumbe
5.
Neema Abdallah
Mjumbe

Kamati ya tathmini ya misaada na maafa ya mfuko:

Kutakuwa na kamati ya tathimini ya mfuko ambayo itakuwa ikikutana mara moja kwa mwezi na pia kukutana kwa vikao vya dharaura itakapo lazimu haja ya kufanya hivyo wakati wowote wa mwanzo wa mwezi  na kwa matukio yoyote ya kati ya mwezi yatakuwa yakisubiri mwisho wa mwezi kwa kingizwa katika agenda za kikao cha mwezi. Pamoja na mambo mengine kamati itawajibika kwa Kamati ya Utendaji ya Mfuko na Itapokea taarifa za maafa na majanga toka kwa kamati ya maafa na kuyafanyia tathimini ya kweli kwa uzito wa janga husika.
Pia itakapokea taarifa za misaada toka kwa kamati ya misaada ya jamii kama itakavyowasilishwa kwake na kuifanyia uchambuzi na tathimini sahihi juu ya misaada inayoombewa fedha/msaada husika.

Kamati hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
Jina
Wadhifa
1.
Sauda Rajabu
Mwenyekiti
2.
Joseph Mwita
Katibu
3.
Victoria Gunze
Mjumbe
4.
Lusajo Kasege
Mjumbe
5.
Fatuma Kilenga
Mjumbe
6.
Esther Daffa
Mjumbe

Kamati ya huduma za kijamii: Kutakuwa na kamati ya huduma za jamii itakayo kutana kila mwezi mara moja na itawajibika kwa kamati ya Utendaji ya Mfuko: Ipatopkea maombi mbali mbali ya misada toka kwa wanachama na kuyajadili kisha kuyatolea mapendekezo yake kwa Kamati ya tathimini ya Misaada na Maaafa ya mfuko kwa utekelezaji wa hatua ya kufanyiwa tathimini juu ya maombi husika. Kamati itafanya uhakiki wa ukubwa wa tatizo la mwanachama linaloombewa misaada kabla ya kuliwasilisha na kulitolea mapendekezo yake kwa kamati ya tathimini ya misaada na maafa ya mfuko.

Kamati hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
Jina
Wadhifa
1.
Devota Elisea
Mwenyekiti
2.
Esther Msechu
Katibu
3.
Fatuma Msigalla
Mjumbe
4.
Alice Kashililika
Mjumbe
5.
Victoria Gunze
Mjumbe
6.
Florence Mariale
Mjumbe
7.
Joyce Samueli
Mjumbe

Kamati ya Nidhamu ya mfuko: Kutakuwa na kamati ya NIDHAMU ya mfuko ambayo pamoja na majukumu yake mengine ya msingi, kamati itakuwa ikikutana mara moja kwa mwezi na kujadili hali ya nidhamu ya wanachama na kuchukuwa hatua za awali juu ya mwanachama atakeyeonekana amekiuka miiko ya uongozi na/au kufanya tendo lolote la kumdhalilisha mwanachama mwenzake, viongozi wake au kwenda kinyume na MAADILI, DIRA, NA DHIMA ya Mfuko.

Kamati hii itakuwa na wajumbe wafuatao:
No.
Jina
Wadhifa
1.
Shaban Kaluse
Mwenyekiti
2.
Lusajo Kasege
Katibu
3.
Fatuma Kilenga
Mjumbe
4.
Saada Myinga
Mjumbe
5.
Devota Elisea
Mjumbe
6.
Emma Sizya
Mjumbe

4.0       AGENDA YA SABA.
Kuteua wajumbe watakaokuwa wanatia sahihi katika benki;
Waliteuliwa wajumbe watatu wa kutia saini katika Benki, mweka hazina anaingia katika orodha hii kwa mujibu wa katiba.
Watia saini ni hawa wafuatao:
No.
Jina
Wadhifa
1.
Shaban Kaluse
Mwenyekiti
2.
Esther Daffa
Mweka Hazina
3.
Devotha Elisea
Katibu Msaidizi

8.0       AGENDA YA NANE.

Mengineyo:
Hapakuwa na hoja zaidi na kila mjumbe aliridhishwa makubalianao hayo.

9.0       AGENDA YA TISA.
Wajumbe walikubaliana kubadilisha kiwango cha michango kwa mwezi, kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 10.000. Hiyo ni kutokana na kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Chodawu Serena Dar es Salaam Ndugu Steven Anthony aliyeshauri tuongeze kiwango cha michango cha mwezi ikiwezekana kiwe shilingi 20,000. Wajumbe walikubaliana na ushauri huo.

10.0    AGENDA YA KUMI.

KUFUNGA KIKAO
Mwenyekiti aliwashukuru  wajumbe wote kwa michango yao ya mawazo katika kikao hicho.
Aliwakumbusha  wajumbe kuweka vyema kumbukumbu za kikao hicho ili kuepusha kusahau maazimio waliyoyafanya wakati wa kikao hicho.

Alitamka kukifunga  rasmi kikao cha 2 cha kikundi cha NGOME IMARA saa 12:00 jioni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...